Leo February 7, 2019 Benki ya Akiba imemaliza nusu ya pili ya mwaka uliyoisha December 2018 kwa kupata faida ghafi yaani Pre-tax profit ya Bilioni 1.2 ikiwa ni ukuaji wa Asilimia 600 ikilinganishwa na kipindi kilichopita cha mwaka 2017, December.
Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi Mtendaji wa ACB Augustine Akowuah amesema ongezeko la faida linatoka na ukuaji wa mikopo ambayo ilitolewa kwa wateja 13,200 wengi wakiwa ni Wafanyabiashara wadogo na kati iliyofikia Bilioni 80.
“Ninafarijika sana matokeo haya nusu ya pili ya mwaka jana, mizania ya malengo yetu tangu mwanzo wa mwaka yametusababisha kuwa na muelekeo mzuri wakati tukigfunga mwaka, tunafurahi mikakati mingi tuliyojiwekea imeleta mabadiliko” Akowuah
“Mwaka 2018 Akiba ilitekeleza mikakati ya kupunguza mikopo chefuchefu, kuimarisha makusanyo ya madeni sugu na utoaji wa mikopo mipya kwa kuzingatia ubora. Hatua tulizochukua ikiwemo kubadilisha na kupitia majukumu na kazi zililenga zaidi kwenye kuimarisha hatari zitokanazo na ukopeshaji” Akowuah
RC MWANRI “NAWAAMBIA WOTE KAA CHONJO, NAONGOZA VICHAA, MATAIRA”