Kocha wa Atletico Madrid Diego Simeone amefunguka na kuitolea ufafanuzi kauli yake iliyosambaa katika video clip kuhusiana nani angemchagua acheze timu yake kati ya Cristiano Ronaldo na Lionel Messi na kunukuliwa akisema angemchagua Ronaldo.
Simeone ameeleza kuwa hakumchagua Ronaldo kwa maana ndio mchezaji bora duniani kuliko Lionel Messi lakini alichomaanisha kama angetaka mchezaji mmoja katika timu yake angemchagua Ronaldo kwa sababu angefiti katika timu yake ila Messi ni mchezaji bora dunia zaidi ya Ronaldo.
“Kama ningeambiwa nichague Ronaldo au Messi nani bora moja kwa moja ningemchagua Lionel Messi, ndio nilisema Ronaldo katika video lakini ni maongezi yalikuwa kati yangu na German Burgos tukizungumzia mpira kama ambavyo wengine wangezungumzia kuhusu hilo”
“Nilipozungumza kuhusiana na Messi na Ronaldo haikuwa katika mtazamo wa maana ya nani bora duniani zaidi ya mwenzake, nilimaanisha kwamba kama unapewa nafasi ya kumsajili mmoja kati ya wachezaji hao katika club ya kawaida Ronaldo ni wazi atafiti”
“Lakini kwa upande wa Lionel Messi amezunguukwa na wachezaji wazuri na Messi ni bora kuliko ya Ronaldo”
Kauli ya Simeone imezua utata baada ya kuonekana awali kumkubali Ronaldo na sio Lionel Messi ambaye ni muargentina mwenzake, baada ya Argentina kupoteza kwa magoli 3-0 dhidi ya Croatia wakati wa World Cup 2018 nchini Urusi walimkosoa sana Messi, hata hivyo Simeone anadaiwa kubadili maneno kutokana na kuambiwa amekosa uzalendo.
“Nimeenda chumbani kwa Canavaro, alichonijibu SINTOSAHAU”-Edo Kumwembe