Taasisi ya Mabalozi wa Usalama Barabarani (RSA) kwa kushiriakiana na Kikosi cha Polisi Usalama Barabarani Mkoani Kilimanjaro wametembelea shule zilizoko pembezoni mwa barabara kuu ili kwa pamoja kushiriakiana katika kutoa Elimu ya Usalama barabarani kwa watoto pomoja na kuanzisha Club’s za Usalama.
Ziara hiyo iliongozwa na Mwenyekiti wa RSA Kilimanjaro Khalid Shekoloa na Kikosi kazi kutoka ofisi ya Kamanda wa Usalama Barabarani Mkoani Kilimanjaro Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Hamadi Hozza na CPL. Maneno Francis.
Ziara hiyo ilijumuisha shule zaidi ya 10 zikiwemo zile zenye wanafunzi wenye mahitaji maalumu Shule zilizotembelewa zipo kwenye Wilaya ya Moshi Mjini, Hai na Moshi Vijinini(Vunjo)
Huu ni mkakati endelevu wa Mabalozi wa Usalama barabarani (RSA) nchi nzima katika kusaidiana na Jeshi la Polisi katika kutokomeza ajali.