Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un ameanza safari yake kwa treni kuelekea nchini Vietnam ambapo atakutana kwa mara ya pili na Rais wa Marekani, Donald Trump.
Kim ameanza safari yake Jumamosi jijini Pyongyang, akiwa ndani ya treni yenye silaha nzito na kusindikizwa na ulinzi mkali ambapo alipita katika ardhi ya China.
Treni hiyo ilionekana ikivuka daraja jijini Beijing na inaelezwa kuwa leo itakuwa ikipitia Magharibi kuelekea Vietnam. Vyanzo vya kuaminika vimeliambia Shirika la Habari la AFP kuwa Kim Jong Un atafika kwenye kituo cha treni cha Dong Dang, kilichoko mpakani Jumanne wiki hii.
Ulinzi mkali umeshuhudiwa katika kituo hicho cha treni cha Dong Dang kuanzia mapema leo asubuhi, kituo hicho kinalindwa na vikosi vya jeshi huku kikiwa kimefungwa kuzuia matumizi ya umma ya kawaida.
Kim Jong Un atawasili katika kituo hicho Jumanne jioni baada ya safari ya Kilometa 4,000 akitumia siku mbili na nusu.
Trump na Kim watakutana February 27 hadi 28, Hanoi nchini Vietnam kwa ajili ya mazungumzo kuhusu makubaliano ya silaha za nyuklia pamoja na mambo mengine ya kiusalama na uchumi kati ya nchi zao ambazo zilikuwa na uhasama kwa miongo kadhaa.
WATANZANIA WANAENDELEA KUJIVUNIA MAMILIONI NA SUPA MZUKA JACKPOT