Leo January 4, 2018 Kesi ya kupinga muswada wa Sheria Mpya ya Vyama vya Siasa iliyofunguliwa na Wanasiasa wa Vyama vya Upinzani imetajwa huku ukiibuka mvutano baina ya Mawakili wa pande zote kuhusu muda wa upande wa mjibu maombi (Serikali) kuwasilisha utetezi wake.
Kesi hiyo imefunguliwa na Kiongozi wa Chama cha ACT- Wazalendo, Zitto Kabwe, na wenzake wawili, Joran Bashange na Salim Biman wote wa Chama cha Wananchi (CUF), kwa niaba ya muungano wa wanachama wa vyama 10 vya upinzani, dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG).