Tarehe January 21, 2019 Spika wa Bunge Job Ndugai ametoa tamko la kumtaka Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali nchini (CAG) Prof. Juma Musa Asaad kufika katika Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge ili akajieleze na kuthibitisha kauli aliyoitoa wakati akifanyiwa mahojiano na chombo kimoja cha habari akiwa nchini Marekani kwa madai kwamba Bunge ni dhaifu na asipofanya hivyo Bunge linauwezo wa kumchukua na kumpeleka kwenye Kamati hata kwa kutumia pingu.