Aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu ameibuka katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa ajili ya kufuatilia kesi , Viongozi wa CHADEMA, akiwemo Mwenyekiti wake Freeman Mbowe.
Nyalandu ambaye alijiuzulu nafasi ya Ubunge Singida Kaskazini alifika Mahakamani majira ya asubuhi na kuudhuria kesi ya uchochezi inayowakabili Viongozi hao.
Mbowe na Matiko walifutiwa dhamana November 23, 2018 kwa madai ya kukiuka masharti ya dhamana na Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri ambaye ameteuliwa kuwa Jaji.