Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika ametangaza rasmi kuwa kutakuwa na Uchaguzi Mkuu wa Viongozi wa Kitaifa na Mabaraza ya Chama hicho utakaofanyika January mwaka 2025 ambapo fomu za kugombea Uongozi ngazi ya Taifa zinapatikana Ofisi za Makao Makuu ya Chama na Mabaraza na Ofisi za Kanda, Mikoa na Wilaya kuanzia December 17,2024 na mwisho wa kurejesha fomu ni January 05,2024 saa 10 jioni.
CHADEMA imeteua wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi kwa kanda mbili.
Mwenyekiti wa Kanda ya Kaskazini, Godbless Lema si miongoni mwa wagombea wa nafasi hiyo kwa kanda hiyo.
Lema alishatangaza siku nyingi kuwa hatogombea katika nafasi hiyo huku jina lake likiwa miongoni mwa yanayotajwa huenda yakawamo katika orodha ya wanaotaka kuwania nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje, John Mrema, uteuzi wa wagombea uongozi kwa Kanda ya Kaskazini na ya Kati, umefanywa na Kamati Kuu ya chama hicho iliyoketi Desemba 14 mwaka huu.
Wagombea walioteuliwa ni kwa nafasi za Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Mtunza Hazina Kanda na mabaraza.