Katibu mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), John Myika, amesema hatagombea ubunge, katika jimbo la Kibamba jijini Dar es Salaam
Mnyika ambaye amekuwa mbunge wa Kibamba ambayo ilikuwa sehemu ya jimbo la Ubungo, kwa miaka 10 mfululizo, amesema amechukua hatua hiyo ili apate muda wa kutosha kutumikia nafasi yake ya sasa ya Katibu Mkuu CHADEMA.
“Haya nilisema kabla ya kuteuliwa kuwa Katibu Mkuu 2019, Nyerere aliwahi kuachia Uwaziri Mkuu akabaki kuimarisha TANU, nami sitagombea ubunge 2020, nitumikie ipasavyo Ukatibu Mkuu CHADEMA tushinde chaguzi.” John Mnyika