Leo July 08 2015 zimebaki saa chache kushuhudia Rais Jakaya Kikwete akivunja Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wapo waliotangaza kwamba wanarudi Majimboni mwao kuomba tena Kura ili Uchaguzi wa August 2015 wapigiwe Kura za kuendelea kuwa Wabunge, lakini wapo walioaga pia.
Mbunge wa Singida Mjini, Mohammed Dewji ni Mfanyabiashara mkubwa lakini pia alikuwa Mbunge wa Jimbo hilo, leo alitua siungida na kuhutubia Wapigakura wake.
Hizi ni Tweets zake alizoandika kile alichowaambia wakati anaaga kutogombea tena Jimbo hilo.
Alhamdulillah I have arrived in #SingidaMjini pic.twitter.com/rJoYzRp9x6
— Mohammed Dewji MO (@moodewji) July 8, 2015
Namshukuru Mweyezi Mungu, wanavikundi vya burudani wote wakiongizwa na Diamond Platnumz na kila aliye fanikisha mkutano huu #SingidaMjini
— Mohammed Dewji MO (@moodewji) July 8, 2015
Baada ya uchaguzi 2005 kipaumbele chetu kilikua ujenzi wa shule za sekondari tulikua na shule 2 na sasa zipo 17. #SingidaMjini
— Mohammed Dewji MO (@moodewji) July 8, 2015
Tumesambaza vyandarua zaidi ya 6000 na hivyo kupunguza vifo vya watoto chini ya miaka 5 na akinamama wajawazito kwa 50% #SingidaMjini
— Mohammed Dewji MO (@moodewji) July 8, 2015
Tumepambana na ugonjwa wa mtoto wa jicho kwa kuleta madaktari bigwa na kutoa miwani kwa zaidi ya wananchi 1000. #SingidaMjini
— Mohammed Dewji MO (@moodewji) July 8, 2015
Tulifanikiwa kujenga wodi ya macho ndani ya Hospitali yetu ya mkoa. #SingidaMjini
— Mohammed Dewji MO (@moodewji) July 8, 2015
Tulifanikiwa kujenga zahanati za Mungumaji na Manga ambazo zimekamilika na zahanati ya Ititi ujenzi unaendelea. #SingidaMjini
— Mohammed Dewji MO (@moodewji) July 8, 2015
Tulifanikiwa kutoa viti vya kubebea wagonjwa katika kituo cha afya cha sokoine na hospital ya mkoa #SingidaMjini
— Mohammed Dewji MO (@moodewji) July 8, 2015
Tulifanikiwa kufunga solar panel pamoja na majokofu ya kutunzia dawa kwenye zahanati za Manga na Unyambwa #SingidaMjini
— Mohammed Dewji MO (@moodewji) July 8, 2015
Tulifanikiwa kuwapeleka wagonjwa kwenye hospitali za rufaa ndani ya nchi na wengine nje ya nchi hasa India. #SingidaMjini
— Mohammed Dewji MO (@moodewji) July 8, 2015
Tulifanikiwa kuchangia ujenzi wa makanisa na misikiti kwa kutoa mabati na sementi na tumechangia michango mingine mingi. #SingidaMjini.
— Mohammed Dewji MO (@moodewji) July 8, 2015
Tumewalipia ada zaidi wa wanafunzi 15,000 ambao wazazi/ walezi walileta maombi. #SingidaMjini
— Mohammed Dewji MO (@moodewji) July 8, 2015
Tulifanikiwa kusambaza madawati katika shule mbalimbali ndani ya jimbo la singida mjini. #SingidaMjini
— Mohammed Dewji MO (@moodewji) July 8, 2015
Tulifanikiwa kutoa zaidi ya vitabu 1,000 kwenye shuke za serikali ndani ya jimbo letu. #SingidaMjini
— Mohammed Dewji MO (@moodewji) July 8, 2015
Tulifanikiwa kuchimba visima viwili ndani ya mtandao wa SUWASA na visima 45 zaidi kwenye vitingoji mbalimbali #SingidaMjini
— Mohammed Dewji MO (@moodewji) July 8, 2015
Tulifanikiwa kusukuma uchimbwaji wa visima 10 – ufadhili wa benki ya dunia na visima 4 – ufadhili wa benki ya BADEA na OPEC. #SingidaMjini
— Mohammed Dewji MO (@moodewji) July 8, 2015
Upatikanaji wa maji safi na salama mwaka 2005 ulikua 23% na sasa ni 81%. Ahsanteni sana kwa ushirikiano wenu. #SingidaMjini
— Mohammed Dewji MO (@moodewji) July 8, 2015
Tumefanikiwa kuongeza mtandao wa barabara za lami katikati ya mji na zinazotoka nje ya mji wetu na tutaendelea kuongeza. #SingidaMjini
— Mohammed Dewji MO (@moodewji) July 8, 2015
Tutaboresha kituo cha mabasi cha Misuna na kuweka taa za barabarani, vivuko vya waendao kwa miguu na mitaro ya maji taka. #SingidaMjini
— Mohammed Dewji MO (@moodewji) July 8, 2015
Hayo ni baadhi ya maendeleo yetu na mimi mbunge wenu nimechangia zaidi ya Sh. BILIONI 5 katika maendeleo ya jimbo letu. #SingidaMjini
— Mohammed Dewji MO (@moodewji) July 8, 2015
Kuwatumikia kwa miaka 10 imekua tunu kubwa sana kwangu na nimejifunza mambo mengi yahusuyo Singida na uongozi kwa ujumla. #SingidaMjini
— Mohammed Dewji MO (@moodewji) July 8, 2015
Nataka mfahamu kuwa dhamira yangu ya kuwatumikia haitokani na nafasi yangu ya Ubunge. Dhamira yangu ni ya uzaliwa. #SingidaMjini
— Mohammed Dewji MO (@moodewji) July 8, 2015
Hivi karibuni niliulizwa “Mhe. Ulikua wapi? ” ni kweli kuwa sasa nimekua na majukumu mengi yanayohitaji muda wangu zaidi. #SingidaMjini
— Mohammed Dewji MO (@moodewji) July 8, 2015
Familia yangu inahitaji muda wangu zaidi na Biashara imekua sana hivi karibuni na hivyo nayo inahitaji muda wangu zaidi. #SingidaMjini
— Mohammed Dewji MO (@moodewji) July 8, 2015
Kutokana na heshima mliyonipa na imani mliyonipa kwa kipindi cha miaka 10 mimi nimeamua kwa kipindi hiki nisigombee. #SingidaMjini
— Mohammed Dewji MO (@moodewji) July 8, 2015
Nipumzike kuwaongoza ili nitoe nafasi kwa kada mwingine wa CCM anipokee kijiti hiki na kuongoza jimbo letu. #SingidaMjini
— Mohammed Dewji MO (@moodewji) July 8, 2015
Maamuzi haya nimeyafanya kwa kuzingatia mahitaji ya Singida na ninaahidi kuendelea kutoa mchango mkubwa zaidi. #SingidaMjini
— Mohammed Dewji MO (@moodewji) July 8, 2015
Ninaahidi kuwa nitendelea kushirikiana na kada wa CCM mtakaye mchagua kuongoza jimbo hili. #SingidaMjini
— Mohammed Dewji MO (@moodewji) July 8, 2015
Pamoja na ahadi yangu na dhamira yangu, utekelezaji wake unategemea sana watu walionizunguka. #SingidaMjini
— Mohammed Dewji MO (@moodewji) July 8, 2015
Nimeanzisha @modewjifoundation na ninaahidi kuweka pesa zaidi kwenye mfuko huu na kuutumia ili kuleta maendeleo #SingidaMjini
— Mohammed Dewji MO (@moodewji) July 8, 2015
Nawashukuru wananchi wote tulioshirikiana kipindi hiki cha miaka 10 nimshukuru Mhe Rais wetu @jmkikwete na viongozi wenzangu #SingidaMjini
— Mohammed Dewji MO (@moodewji) July 8, 2015
Ninashukuru kwa nafasi mliyonipa na ninaomba radhi pale ambapo nimewakosea. Ahsanteni kwa kunisikiliza. #SingidaMjini
— Mohammed Dewji MO (@moodewji) July 8, 2015
I love you #SingidaMjini 😥 pic.twitter.com/nWfg5EYfa9
— Mohammed Dewji MO (@moodewji) July 8, 2015