Klabu ya AS Monaco ya Ligi Kuu ya Ufaransa imefikia makubaliano na Southampton kwa ajili ya kumsajili beki wa Ghana Mohammed Salisu.
Hatua hiyo inatokana na mchezaji huyo kufikia makubaliano na klabu juu ya masharti ya kibinafsi pamoja na kukamilisha vipimo vya lazima vya afya.
Salisu alitatizika msimu uliopita wakati akiwa na Saints msimu uliopita kutokana na jeraha na hakuonekana katika sehemu ya mwisho ya msimu huku klabu hiyo ikishuka daraja.
Beki huyo wa kati wa Black Stars alicheza mara 22 kwenye Premier League msimu uliopita.
Mghana huyo amebakiza mwaka mmoja tu kwenye mkataba wake wa sasa kwenye Uwanja wa St Mary’s lakini kuna uwezekano akaishia Ufaransa msimu huu wa joto.
Mchezaji huyo hapo awali alikuwa kwenye rada za Fulham ya Ligi Kuu ya Uingereza, ambayo iliamua kumsajili Calvin Bassey kutoka Ajax mbele ya Salisu.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 hakujumuishwa kwenye kikosi cha Southampton kwa ajili ya mechi zao za kirafiki za kujiandaa na msimu mpya dhidi ya AZ Alkmaar Jumamosi au Bournemouth Jumanne wakati anakaribia kuondoka.
Mohammed Salisu atakamilisha vipimo vya afya kama mchezaji mpya wa AS Monaco leo na mara tu baada ya hapo, Axel Disasi ataruhusiwa kukamilisha matibabu na Chelsea 🔵🇫🇷
Salisu anajiunga na Monaco kwa dili la €15m kutoka Southampton.