Mahakama ya hakimu mkazi katika eneo la Yaba katika Jimbo la Lagos imewaweka rumande Azeez Fashola, maarufu kama Naira Marley, na sosholaiti wa Lagos Balogun Eletu, anayejulikana pia kama Sam Larry.
Wawili hao watakaa rumande kwa siku 21.
Kamanda wa Polisi wa Jimbo la Lagos walikuwa wameomba kufungwa kwa siku 30 kwa Fashola na wengine ili kukamilisha uchunguzi wao unaoendelea.
Hata hivyo, Hakimu Adeola Olatunbosun aliamua kwamba kifungo cha siku 21 kinatosha.