Meneja Ustawi wa Jamii na Uhusiano wa taasisi ya Tiba ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu (MOI) Jumaa Almas ametoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari leo August 04 2016 jijini Dar es Salaam juu ya tuhuma zilizotolewa na baadhi ya vyombo vya habari kuwa taasisi hiyo inabana matumizi na kusababisha msongamano wa wagonjwa taasisi hiyo.
Amesema idadi ya wagonjwa wa upasuaji katika taasisi hiyo imeongezeka kutoka wagonjwa 20 mpaka wagonjwa 40 kwa siku ambapo 80% ya wagonjwa walio katika taasisi hiyo wanahitaji upasuaji wa dharura jambo ambalo limeilazimu taasisi hiyo kufungua wodi nyingine ya upasuaji ili wagonjwa wote wanaohitaji huduma ya upasuaji wa dharura waweze kufanyiwa ili kuokoa maisha yao.
>>>’Msongamano wa wagonjwa MOI hausababishwi na kubana matumizi bali ni kutokana na kuongezeka kwa wagonjwa kutoka wagonjwa 20 mpaka wagonjwa 40 kwa siku ambapo kumesababishwa na ongezeko kubwa la ajali hasa za pikipiki katika jiji la Dar es Salaam’
Amefafanua kuwa wagonjwa wa upasuaji wa kichwa na ubongo hulazimika kusubiri kwa muda kutokana pindi wanapopelekwa katika chumba cha wagonjwa mahututi mara baada ya upasuaji na kuongeza kuwa vyumba vya wagonjwa mahututi ni vichache ikilinganishwa na ongezeko kubwa la wagonjwa wanaohitaji upasuaji huduma hiyo.
Ameongeza taasisi hiyo inategemea kuongeza vyumba vingine zaidi kwa ajili ya wagonjwa mahututi ili kukidhi idadi ya wagonjwa ambao wamekuwa wakiongezeka kila siku.
ULIKOSA HAYA MANENO YA POLISI SINGIDA BAADA YA KUMKAMATA TUNDU LISSU? BONYEZA PLAY HAPA CHINI