Nchini Afrika Kusini, Wizara ya Sheria ilitangaza Ijumaa, Januari 5, kufunguliwa tena kwa mojawapo ya kesi zinazojulikana zaidi za mauaji ya wanaharakati weusi chini ya utawala wa ubaguzi wa rangi. “Cradock Four”, iliyopewa jina la mji wao kusini mwa nchi, walikuwa wapigania uhuru wanne ambao miili yao ilipatikana ikiwa imechomwa moto na kukatwakatwa mnamo mwaka 1985.
Tangazo hili lilikaribishwa na familia za wahanga lakini linakuja na mfadhaiko, kwani karibu miaka arobaini imepita tangu uhalifu huu utekelezwe.
“Mshukiwa wa mwisho alifariki dunia hivi karibuni. Hakuna aliyebaki kujibu maswali yetu. Hata hivyo, baada ya mwaka 1994, kulikuwa na matumaini ya kufunguliwa mashtaka. Kamwe hawakulipa kwa matendo yao ya kikatili. Haya yote yanatusikitisha sana,” anasema Nombuyiselo, mjane wa Sicelo Mhlauli, mkuu wa shule wa zamani na mwanaharakati aliyeuawa wakati huo akiwa na umri wa miaka 39 pamoja na wanaume wengine watatu.
Tayari kumekuwa na chunguzi mbili uliofanywa katika miaka ya 80 na 1990 karibu kuhusiana na suala hili lakini bila matokeo. Kisha wajumbe wa vikosi vya usalama walikubali wajibu wao mbele ya Tume ya Ukweli na Maridhiano … na ombi lao la msamaha lilikataliwa, kwa sababu ya kukiri kutokamilika, lakini tangu wakati huo, hakuna mashtaka yoyote yaliyoanzishwa.