Makao ya mfalme wa Morocco Jumatano yamesema kwamba taifa hilo litatumia takriban dola bilioni 11.7 za kimarekani ndani ya miaka 5 ijayo, kufanya ukarabati kutokana na uharibifu ulioyosababishwa na tetemeko la ardhi la hivi karibuni.
Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, mpango huo unalenga watu milioni 4.2 kutoka kwenye maeneo yalioathiriwa zaidi ya Al Haouz, Chichaoua, Taroudant, Marrakech, Qourzazate na Azizlal, kulinagana na taarifa kutoka makao ya mfalme, kufuatia mkutano kati ya Mfalme Mohammed VI, na maafisa wa serikali na wa jeshi.
Mpango huo inahusisha miundombinu mipya inayoendana na maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwenye maeneo yalioathiriwa na tetemeko la ardhi, taarifa hiyo imeongeza. Taarifa zimeongeza kusema kwamba mpango huo utafadhiliwa na serikali, msaada wa kimataifa, pamoja na mfuko maalum uliobuniwa baada ya mkasa huo.
Tayari dola milioni 700 zimepokelewa kwenye mfuko huo.
Mpango huo ungelenga watu milioni 4.2 katika majimbo yaliyoathiriwa zaidi ya Al Haous, Chichaoua, Taroudant, Marrakesh, Ouarzazate na Azizlal, ikulu ya kifalme ilisema Jumatano, kufuatia mkutano wa Mfalme Mohammed VI na maafisa wa serikali na jeshi.