Rais wa Shirikisho la soka Afrika CAF Patrice Motsepe amelipongeza Shirikisho la soka nchini Morocco (FRMF) kwa ujenzi na uzinduzi wa Ofisi za Kisasa zaidi kwa Mashirikisho ya soka Afrika.
Motsepe ametoa pongezi hizo kwa Rais wa FRMF, Faouzi Lekja pamoja na Serikali ya Morocco inyoongozwa na Mfalme Mohammed wa sita ambaye ametia nguvu zaidi kukuza soka la Taifa hilo.
“Tunapenda kuwapongeza wenzetu kutoka Morocco pamoja na Serikali yao kwa kazi nzuri wanayofanya ambayo inatupa jina zuri kama Waafrika katika soka Duniani”>>>> Motsepe
Morocco wameendelea kuweka uwekezaji mkubwa zaidi kwenye soka ikiwa ni sehemu ya kujiandaa na kuishawishi FIFA ikubali kuipa ridhaa ya kuwa Taifa pili kutokea Afrika kuandaa fainali zao Kombe la Dunia 2030 baada ya Afrika Kusini kuwa Taifa la kwanza kutokea Afrika kuwahi kuandaa fainali hizo kwa mara ya kwanza 2010.