Shirikisho la soka la Morocco linaendesha kozi ya ukocha maalum kwa makocha wanaosaka Leseni A ya Caf kozi ambayo inaendelea huko Agadir ikiwa imeanza toka Juma na nusu lililopita.
Kozi inahusisha makocha toka nchi kadhaa za Afrika wakiwemo wachezaji wa zamani wa kimataifa waliotumikia timu za taifa za Morocco na Nigeria.
Idadi kamili ya makocha hao ni 30 wakiwemo wachezaji wa zamani 25 walioichezea Morocco huku akiwemo mshambuliaji wa zamani wa Everton na Super Eagles Daniel Amokachi.
Mataifa mengine ambayo makocha wake wamefuzu kozi hiyo ni Togo pamoja na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo ambapo makocha hao wamekuwa wakipitia mafunzo ya nadharia na vitendo yakiongozwa na wakufunzi toka UEFA na CAF.
Katika kozi hizo makocha wamekuwa wakikutanishwa na wanasaikolojia ambao wamekuwa sehemu ya mafunzo hayo ambauo hayakujikita kwenye masuala ya michezo pekee bali mafunzo ya kijamii na maisha kwa jumla.
Kwa muda mrefu baadhi ya mataifa wanachama wa Caf yameshindwa kuandaa kozi za Leseni A kwa makocha wake hali inayomaanisha kuwa Morocco imeendekea kuwa mchango mkubwa kwa maendeleo ya soka la Afrika.