Shirika la Kiserikali la Nchini Morocco limetoa vibali 10 vya kwanza vya uzalishaji wa bangi kwenye viwanda kwa ajili ya dawa na biashara katika nchi za nje, kama matokeo yalioletwa na mabadiliko ya sheria iliyopitishwa mwaka jana.
Wakulima waliopo katika Vyama vya Ushirika katika maeneo yaliopo kwenye milima ya kaskazini mwa Al Houceima, Taounat na Chefchaouen wataruhusiwa kulima bangi ili kukidhi mahitaji ya soko halali.
Bangi tayari inalimwa kwa wingi Morocco kinyume na sheria, huku sheria mpya iliyopitishwa na Bunge la nchini humo hairuhusu matumizi yake kama starehe.
Sheria hiyo inanuiwa kuboresha mapato ya Wakulima na kuwalinda dhidi ya walanguzi wa dawa za kulevya ambao wanadhibiti biashara ya bangi na kuisafirisha kinyume cha sheria kwenda nchi za Ulaya.
ACHOMWA VIBAYA NA UJI KISA KALA MAHARAGE KIJIKO KIMOJA, MAMA YAKE AFUNGUKA “SHANGAZI KAHUSIKA”