Wiki iliyopita tu, ripoti ya Umoja wa Mataifa ilisema hali ya haki za binadamu nchini Urusi “imezorota kwa kiasi kikubwa” tangu uvamizi wake nchini Ukraine.
Wiki sita baada ya uvamizi huo wa Ukraine, baraza kuu la Umoja wa Mataifa lilisimamisha kiti cha Urusi katika baraza la haki za binadamu la nchi 47 mjini Geneva.
Urusi sasa inaripotiwa kutaka kujichagulia tena kwenye baraza hilo katika kura ambayo itaonekana kama mtihani wa kiwango cha uungwaji mkono ambao taifa hilo linahifadhi kimataifa.
Kupitia ripoti za BBC zinasema zimepata nakala ya karatasi ya msimamo ambayo Urusi inazunguka kwa wanachama wa Umoja wa Mataifa kuomba uungwaji mkono wao katika kura ya mwezi ujao.
Hati iliyoonekana na BBC inasemekana kujumuisha nadhiri kutoka Urusi ya kutafuta “suluhu za kutosha kwa masuala ya haki za binadamu” na kukomesha baraza hilo kuwa “chombo kinachotumikia matakwa ya kisiasa ya kundi moja la nchi”.