Waziri wa Mambo ya Ndani, George Simbachawene amesema tukio la ajali ya moto katika Soko Kuu la Biashara Kariakoo linapaswa kuwa fundisho juu ya kujikinga na majanga ya moto, huku akiwata Wakuu wa Mikoa yote nchini kulitumia Jeshi la Zimamoto kufanya ukaguzi katika maeneo yote ya mikusanyiko ya watu.
Waziri Simbachawene ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam alipotembelea Soko la Kariakoo ambalo liliungua kwa moto usiku wa July 10, 2021.