Jeshi la Zimamoto na Uokoaji limesema hakuna madhara kwa Binadamu yaliyotokea kutokana na moto uliozuka Kiwanda cha kuzalisha plastiki cha Jambo 11 kilichopo Vingunguti Jijini Dar es salam lakini mashine na malighafi zimeungua na hadi sasa magari ya Zimamoto tisa yapo eneo la tukio kuendeleza mapambano ya kuuzima moto huo.
Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Ilala, Elisha Mugisha amenukuliwa akisema “Malighafi inayotumika kutengeneza plastiki na mashine zinazozalisha ndizo zinazoungua, tulichofanya ni kuzuia mashine ambazo hazijaathirika zisiungue na tumedhibiti moto usiende ghala jingine”