Watu walioshiriki ibada ya kuaga mwili wa Mhubiri wa Kimataifa, Temitope Balogun Joshua maarufu TB Joshua wamepata taharuki baada ya kutokea mlipuko walipokuwa katika Kanisa kuu la Kikristo la mataifa lililopo Lagos, Nigeria.
Mjane wa marehemu, Evelyn Joshua aliongoza waombolezaji wapatao 6,000 katika maandamano ya taa ili kuashiria mwanzo wa ibada ya mazishi ya mhubiri huyo wa Nigeria aliyefariki dunia Juni 5, 2021 siku chache kabla ya kusherehekea kumbukumbu ya siku yake ya kuzaliwa. Joshua atazikwa Julai 9, 2021.
Wakati shughuli ya kuaga mwili ikiendelea jijini Lagos, moto ulizuka katika majengo ya kanisa hilo majira ya saa 11 jioni.
Taarifa iliyotolewa na uongozi wa kanisa hilo inaeleza kuwa moto ulisababishwa na cheche ya umeme na kwamba tukio hilo lilidhibitiwa haraka na hakuna aliyejeruhiwa.
“Tunamshukuru Mungu kwa kuendelea kutulinda, tunawahakikishia umma kwa ujumla kuwa hakuna sababu ya kuwa na wasiwasi na huduma za kusherehekea maisha ya Nabii TB Joshua zitaendelea kama ilivyopangwa,”