Yakiwa yamebakia masaa takribani matano kabla ya mechi ya kugombea ufalme wa jiji London katika Chelsea dhidi ya Arsenal kuchezwa, millardayo.com inakuletea rekodi ya makocha wanaoziongoza timu hizo Jose Mourinho wa Chelsea dhidi ya Arsene Wenger wa Gunners.
Kwa mujibu wa rekodi zilizotolewa na BBC – Wenger amekutana na Mourinho wamekutana mara 11 katika mechi za Barclays Premier League.
Katika mechi hizo 11 – Mourinho ameiongoza timu ya Chelsea kushinda mara 6 na kutosa sare 5, huku Wenger akiwa hajawahi kuambulia ushindi dhidi ya mpinzani wake.
Wenger ameiongoza Arsenal kufunga jumla ya magoli sita dhidi ya Chelsea – wakati Mourinho ameiongoza Chelsea kufunga jumla ya magoli 19 dhidi ya Gunners.
Je leo Mourinho ataendeleza ubabe dhidi ya Wenger – au mambo yatakuwa tofauti na Wenger atafuta uteja dhidi ya Mou? Majibu tutayapata hapa hapa jioni ya leo.