Movie mpya ya Mwigizaji wa Tanzania Idris Sultan iitwayo “MARRIED TO WORK” imeingia kwenye tano bora ya filamu zinazo-trend kwa sasa kwenye NETFLIX ikiwa ni ndani ya wiki moja tu toka ianze kuoneshwa kwenye mtandao huo.
Ni Filamu yenye stori nzuri ya kusisimua itayokufanya utamani kutazama itaishaje ambapo Ili kuokoa biashara yao ya nyumba na makazi, itamlazimu Mwanamke Mpambanaji pamoja na Boss wake kumuaminisha Mwekezaji kwamba wawili hao wamefunga ndoa licha ya ukweli kwamba hakuna ndoa na hata hawapendani.
Ndani ya filamu hii waliohusika ni Waigizaji kutoka Tanzania, Kenya na Nigeria ambapo waliohusika kwenye utengenezaji ni Wakenya huku pia Muongozaji wake akiwa ni Mkenya.