Michuano ya Kombe la Mapinduzi imeendelea tena usiku wa January 3 baada ya kuchezwa mchezo wa awali kati ya Dar Es Salaam Young African ya Tanzania bara dhidi ya Mafunzo FC ya visiwani Zanzibar, baada ya mchezo huo kupigwa na Yanga kuibuka na ushindi wa goli 3-0.
Usiku wa January 3 ulichezwa mchezo wa pili wa Kundi B ambapo unajumuisha timu za Yanga, Mafunzo, Mtibwa Sugar na Azam FC. Usiku huo ulikuwa ni zamu ya kupigwa mchezo kati ya Azam FC dhidi ya Mtibwa Sugar, ikiwa wiki moja nyuma zilikutana katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania bara na Azam FC kuibuka na ushindi wa goli 1-0.
January 3 katika mchezo ambao Mtibwa Sugar walikuwa wanapewa nafasi ya kulipiza kisasi kwa kuifunga Azam FC, wamekubali kutoka sare ya goli 1-1. Mtibwa walianza kupachika goli dakika ya 61 kupitia kwa Hussein Javu, goli ambalo lilikuja kusawazishwa na John Bocco kwa mkwaju wa penati dakika ya 74 baada ya kufanyiwa madhambi. Hivyo Yanga atakuwa anaongoza kundi kwa kuwa na point 3 na magoli matatu.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.