Mpango Mkakati wa Taifa wa Huduma Jumuishi za Fedha wa 2023 – 2028 ni Mpango wa tatu kutekelezwa chini ya Baraza Ia Taifa Ia Huduma Jumuishi za Fedha. Mpango huu ni mwendelezo wa mafanikio yaliyofikiwa chini ya utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Pili ambao utekelezaji wake ulikamilika Desemba 2022.
Katika utekelezaji wa Mkakati wa pili wa Taifa wa Huduma Jumuishi za fedha,Tanzania imepata mafanikio makubwa yakiwemo ongezeko la asilimia ya watu wazima waliofikiwa na huduma rasmi za fedha kutoka asilimia 86 mwaka 2017 hadi 89 mwaka 2023. pamoja na ongezeko la watu wazima wanaotumia huduma rasmi za fedha kutoka asilimia 65 mwaka 2017 hadi asilimia 76 mwaka 2023. Kwa kiasi kikubwa.
Mafanikio haya yamechagizwa na kuongezeka kwa matumizi ya huduma za fedha kwa njia ya kidijitali. uelewa wa huduma za fedha kwa watumiaji. na ushirikiano kati ya wadau wa huduma jumuishi za fedha wa sekta ya umma na binafsi.
Katika Mpango wa dira yetu ni kuona rika Ia watu wazima na wafanyabiashara wote wanafikiwa na kutumia bidhaa na huduma mbalimbali za fedha zenye ubora wa hali ya juu iii kuboresha ustawi wa maisha yao ya kila siku. Ili kufanikisha utekelezaji wa malengo tuliyojiwekea. Mkakati huu utatekelezwa kwa ushirikiano wa sekta ya umma na binafsi.
Mpango huu umeweka mikakati mahsusi ya kuongeza idadi ya wananchi wanaotumia huduma za fedha kutoka katika makundi maalumu kama wanawake. vijana. wajasiriamali wadogo na wa kati. wakulima wadogo. wavuvi na watu wenye mahitaji maalumu iii kuongeza ushirikishwaji wa makundi hayo katika shughuli za kiuchumi na kuongeza mchango wake katika maendeleo ya uchumi wa Taifa.
Utekelezaji wa Mpango huu pia utasaidia watumiaji wa huduma za fedha nchini kufikiwa na watoa huduma iii kuwapa fursa ya kutumia aina mbalimbali za bidhaa na huduma fedha zilizo na ubora wa hali ya juu. Ili kufikia azimio hili. Serikali na sekta binafsi tutashirikiana kuweka mazingira wezeshi kwa watoa huduma za fedha na kuongeza matumizi ya teknoiojia katika kufikisha huduma za fedha kwa wananchi.
Nimatarajio yangu kuwa taasisi za umma na za binafsi zinazotekeleza Mpango huu. zitaendelea kushirikiana na wadau wa huduma jumuishi za fedha nchini iii kufikia malengo tuiiyojiwekea kwa nia ya kuleta ustawi wa sekta ya fedha na kufikia uchumi jumuishi nchini.