Kremlin inasema Putin hana mpango wa kuhudhuria mkutano wa G20 nchini India mnamo Septemba ana kwa ana.
Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) imetoa hati ya kukamatwa kwa Putin ikimtuhumu kwa uhalifu wa kivita nchini Ukraine, shtaka ambalo Kremlin inakanusha vikali.
Lakini, India si nchi mwanachama wa ICC.
Wiki hii Putin alihudhuria mkutano wa viongozi kutoka kundi la BRICS la mataifa yanayoinukia kiuchumi nchini Afrika Kusini kwa njia ya video.
Msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov alisema muundo wa ushiriki wa Putin utajulikana baadaye.
Putin alihudhuria mkutano wa kilele wa BRICS uliomalizika hivi majuzi nchini Afrika Kusini kwa njia ya video. Aliwakilishwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergey Lavrov.
India ndio mwenyeji wa toleo la sasa la Mkutano wa G20 na hafla kuu itafanyika New Delhi mnamo Septemba 9-10. Mkutano huo huenda ukahudhuriwa na wakuu 29 wa nchi pamoja na maafisa wakuu wa EU na nchi zilizoalikwa na wakuu 14 wa mashirika ya kimataifa.
Tamko la Viongozi wa G20 litapitishwa mwishoni mwa Mkutano wa New Delhi.