Kamati ya Olimpiki ya Kimataifa imepinga mpango wa Ufaransa wa kupiga marufuku vazi la hijabu katika michezo ya Olimpiki ya Paris 2024.
Siku chache baada ya hatua tata ya Waziri wa Michezo wa Ufaransa, Amelie Odia-Castera, Kamati ya Olimpiki ya Kimataifa imetangaza kwamba, hakutakuwa na vikwazo vya hijab kwa wanariadha katika Michezo ya Olimpiki ya Paris, ambayo itafanyika Julai 26 hadi Agosti 11, 2024.
Hapo awali, Ofisi ya Haki za Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa ilikosoa uamuzi wa serikali ya Ufaransa wa kupiga marufuku vazi la hijab kwa wanariadha wa Ufaransa katika Michezo ya Olimpiki ya 2024 mjini Paris.
Katika taarifa yake, Kamati ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa, ililaani marufuku ya vazi la hijabu nchini Ufaransa, ikisema kuwa nchi hiyo imekiuka mkataba wa kimataifa wa haki za binadamu kwa kuwazuia wanawake na wasichana kuvaa hijabu shuleni na maeneo ya umma.
Kamati ya Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa ilitoa taarifa hiyo baada ya Waziri wa Michezo wa Ufaransa kusema Jumapili iliyopita kwamba, wanariadha wa Ufaransa hawataruhusiwa kuvaa hijabu katika Michezo ya Olimpiki ya mwaka ujao mjini Paris.