Mpango maalum wa Unywaji maziwa mashileni umezinduliwa katika shule ya msingi Ubungo Plaza lengo likiwa ni kuhakikisha watoto wanakunywa maziwa wakiwa mashuleni.
Akizungumza katika uzunduzi huo katika shule ya Msingi Ubungo Plaza Katibu tawala wa Uchumi mkoa wa Dar es Salaam Dkt Elizabeth Mshote amesema shule zilizofikiwa katika mkoa wa Dar es Salaam hadi sasa ni shule 8 ambacho ni kiasi kidogo kutokana na shule zilizopo katika mkoa huo na kulinganisha na uhitaji wa lishe bora kwa wanafunzi kwasababu lishe bora inasaidia ufahamu kwa wanafunzi hivyo zoezi hilo litaendelea katika shule zote katika mkoa Dar es Salaam.
George Msalya ni msajili wa bodi ya maziwa amesema mpango huu wa unywaji maziwa mashuleni utaenda kabisa kumaliza tatizo la udumavu hususani kwenye makundi ya watoto.
Hatahivyo mkuu wa Mradi wa Global Alliance Dkt WinFrida Mayilla amesema watoto wakinywa haya maziwa watapata virutubishi vyote ambavyo vina umuhimu na ambavyo vitamsaidia mtoto na amewataka wazazi , waalimu pamoja na jamii waamasishe watoto kula vyakula kama maziwa ambavyo vitaleta afya bora .
“ Watoto wana udumavu , watoto wana lishe duni hivyo tunakwenda kutumia hii bidhaa hii ya maziwa hasa kwenye makundi haya ya watoto na maziwa haya ni bora na salama kabisa na yana virutubishi ambavyo itafanya miili na akili iweze kukua vizuri “ amesema WinFrida .