Rachel Ghannouchi, mwenye umri wa miaka 81 na spika wa zamani wa bunge, alikamatwa mwezi uliopita kwa tuhuma mbalimbali, kama sehemu ya kile ambacho shirika la Human Rights Watch lilikitaja wiki iliyopita kama hatua ya kudhibiti chama kikuu cha siasa nchini humo.
Ghannouchi ni miongoni mwa zaidi ya wapinzani 20 wa kisiasa wa Saied, wakiwemo mawaziri wa zamani na wafanyabiashara waliokamatwa tangu Februari.
Alifikishwa mahakamani mwishoni mwa mwezi Februari kutokana na mashtaka yanayohusiana na ugaidi baada kushutumiwa kuwaita maafisa wa polisi “wadhalimu.”
Kesi hiyo ni moja ya kesi zilizofunguliwa na mamlaka dhidi ya Ghannouchi, ambaye chama chake cha Ennahda cha mrengo wa Kiislamu ndicho kilikuwa chama kikuu bungeni kabla ya rais Saied kulivunja bunge mwezi Julai mwaka wa 2021 na kujinyakulia madaraka yaliyomruhusu kutawala kwa amri ya kiutendaji.
Kukamatwa kwake mwezi uliopita, pamoja na wengine, kulizua wasiwasi wa kimataifa, huku Umoja wa Ulaya ukikumbusha umuhimu wa “maadili ya msingi” ya wingi wa vyama vya siasa.
Marekani ilisema kumakatwa kwa watu hao kunaashiria “hali inayozidi kuwa mbaya ya vitisho vinavyofanywa na serikali ya Tunisia dhidi ya wanaodhaniwa kuwa wapinzani.”