Hii nyingine nayo kutoka Bungeni.. Mbunge Idd Azzan wa Kinondoni Dar kaingia kwenye headlines wakati anachangia Bunge la Bajeti.. Story za uhalifu ni nyingi sana Dar, yeye kalizungumzia hilo leo.
“Hatuwezi kujisifu kwamba sisi ni kisiwa cha amani wakati leo kuna viashiria vya kuvunjika kwa amani.. matokeo ya ugaidi na ujambazi kupita kiasi vinaonekana.. Polisi wamezidiwa ama kwa sababu hawana vitendea kazi au kwa sababu ni wachache.. Niwapongeze askari wa Kinondoni pamoja na RPC Wambura kwa kazi nzuri wanayoifanya kupambana na uhalifu pamoja na kwamba hawana vitendea kazi na askari ni wachache>> Mbunge Idd Azzan.
“Naiomba Serikali iangalie Polisi Kinondoni kutokana na hali halisi ilivyo ni Wilaya yenye watu wengi sana, bahati mbaya sana nyie viongozi wote mnaishi Kinondoni na mnatakiwa mlindwe sasa utajiuliza Askari wangapi watalinda wananchi, wangapi watakwenda kulinda viongozi.. Bajeti hii isipite kama pesa hazikuongezwa”>> Idd Azzan.
Nimekuwekea hapa sauti yote ya Mbunge huyo, ukiplay utamsikia Idd Azzan wakati akichangia Bungeni.