Mwenyekiti wa Kamati ndogo ya Utaliii na usimamizi wa wanyama pori, Mbunge Dkt Shogo Mlozi Sedoyeka ameandaa ziara ya Wabunge wa Afrika Mashariki, Kamati ya Kilimo, Utalii na Maliasili kutembelea Hifadhi ya Ngorongoro, Arusha, Tanzania katika mkakati wa kutangaza EAC kama kivutio kimoja cha utalii (Single travel destination).
Amesema atatumia nafasi yake kuhakikisha Wabunge wa EAC wanaendelea kutangaza vivutio katika nchi zote wanachama kuongeza idadi ya watalii na kuwaletea tija zaidi wana EAC katika sekta ya utalii na sekta zingine zinazoshikana na utalii.
Aidha, Mbunge huyo amesema takwimu inaonesha EAC imevutia watalii 6.95M mwaka 2019 kabla ya COVID 19, idadi hiyo ni ndogo ukilinganisha na fursa zilizopo
Hivyo mkakati huo unalenga kuongeza idadi ya watalii wanaotembelea EAC. Pia Mbunge huyo aliongeza kuwa ziara hii imesaidia kuona shughuli za uhifadhili, mafanikio na changamoto zake nchini Tanzania na kutumia uzoefu huo katika kutoa ushauri wa kisera EAC.
Ziara hii imefadhiliwa na The Fungua Trust kwa kushirikiana na Hifadhi ya Ngorongoro na Tanzania Association of Tour Operators.