Bado michuano ya Kombe la Mapinduzi inaendelea visiwani Zanzibar, baada ya jioni ya January 4 kupigwa mchezo wa kwanza wa Kundi A kati ya URA ya Uganda dhidi ya JKU ya Unguja, usiku wa January 4 ukapigwa mchezo wa pili wa Kundi A kati ya Simba ya Dar Es Salaam na Jamuhuri ya Pemba.
Mchezo wa Simba dhidi ya Jamuhuri katika dimba la Amaan ulikuwa wa kuvutia kwa kiasi kikubwa, kwani kwa dakika zote timu zote zilikuwa zinacheza mpira kabla ya dakika za mwishoni Simba kuutawala mchezo, mchezo ulianza kwa Simba kufunga goli la mapema kupitia kwa Awadh Juma dakika ya 13.
Goli la Simba lilidumu kwa dakika tatu pekee, kwani dakika ya 16 Mwalimu Mohamed alifanikiwa kuisawazishia Jamuhuri, kikosi cha Jamuhuri baada ya kurudi mapumziko kilifanikiwa kufunga goli la pili kupitia kwa Ame Hamisi Bangaseka dakika ya 53.
Kufuatia Jamuhuri kuongoza kwa goli 2-1 walianza kucheza mpira wa kujihami zaidi, kitu kilichowafanya Simba kuwashambulia zaidi na Awadhi Juma dakika ya 73 akaisawazishia Simba na kufanya mchezo umalizike kwa sare ya goli 2-2. Kwa sasa Kundi A litakuwa linaongozwa na URA nafasi ya pili watakuwa Simba na Jamuhuri, wakati JKU wakiambulia kushika mkia.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.