Jumatatu ya January 4 ni siku ambayo Kombe la Mapinduzi liliendelea tena kwa mchezo wa kwanza wa Kundi A kuchezwa katika uwanja wa Amani Zanzibar. Huu ulikuwa ni mchezo wa tatu wa mashindano na wa kwanza kwa Kundi A ambalo lina timu za Simba, Jamuhuri, JKU na URA ya Uganda.
Hivyo timu ya URA dhidi ya JKU ndio zilikuwa timu za kwanza kufungua mchezo wa mechi za Kundi A, wakati Simba na Jamuhuri wakisubiri saa 20:15 kukutana katika mchezo wa pili wa kundi hilo. Mchezo wa URA ya Uganda dhidi ya JKU ya Unguja ulianza kwa URA kupata goli la uongozi dakika ya 12 kupitia kwa Agaba Oscer.
JKU walikuja juu na kufanikiwa kusawazisha goli hilo dakika ya 18 kupitia kwa Mohamed Abdallah, ila furaha ya suluhu yao haikufanikiwa kudumu, kwani URA walifunga goli la pili kupitia kwa Oramchan Villa dakika ya 21 na dakika ya 77 Oramchan Villa akapchika goli la tatu kwa URA na kufanya mchezo kumalizika kwa 3-1. Kwa matokeo hayo URA watakuwa wanaongoza Kundi A kwa point tatu na magoli matatu.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.