Tunayo stori kutokea kwa Mwenyekiti wa chama cha NCCR Mageuzi, James Mbatia ambapo amezungumza maneno mawili mbele ya Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan kuhusu haki za walemavu.
Mbatia ambaye ni Mbunge wa Vunjo ameyasema hayo wakati akitoa tuzo ya Mwanasiasa zilizoandaliwa na Mwenyekiti wa IPP, Regnald Mengi ambapo amesema alichokifanya Mengi ameweza kudumisha, kutetea na kulinda utu, heshima na haki msingi za watu wenye ulemavu.
“Sio binadamu wa kawaida anayeweza kufanya hivyo kwa wale wenye ulemavu wa nje walio wengi tumeamua kuwaita kana kwamba hawajakamilika, hapana binadamu yoyote aliyeumbwa na Mwenye Mungu amekamilika kwa ndani ila sisi tuliokamilika kwa nje kwa ndani tuna ulemavu wa hali ya juu ya kifikra,“amesema