Naibu waziri wa Fedha, Hamad Chande amesema wananchi wa Kiuyu kigongoni wilaya ya Wete mkoa wakaskazini Pemba wanatarajia kunufaika na huduma za afya zitakazotolewa katika kituo cha afya cha kisasa kinachojengwa katika eneo hilo.
Naibu waziri Chande amesema hayo kisiwani Pemba baada ya kutembelea na kukagua ujenzi wa kituo hicho ambapo amesema pamoja na changamoto zilizokuwepo ameridhishwa na kasi ya utekelezwaji wa mradi huo.
Kwa upande wake mhandisi anaye simamia mradi huo Sabra Seif Suleiman kutoka wakala wa majengo Zanzibar anasema jengo hilo lina vyumba vine vya kulaza wagonjwa pamoja na vyumba 18 vya ofisi.
“Gharama za mradi huu ni zaidi ya bilioni moja na milioni saba,”.