Ni wiki imepita kwa mchungaji wa kanisa la mlima wa moto Assemblies of God , Mikocheni ‘B’ Dr. Getrude Lwakatare kutoa milioni 25 kuwalipia wafungwa ambao walikosa fedha kulipia faini na kufungwa jela.
September 15 2016 mwenyekiti wa bodi ya Parole Taifa Augustino Mrema amependekeza kufanyika kwa harambee kwa makanisa yote Tanzania.
Mrema ameomba makanisa yote kutoa sadaka ya siku moja ya Jumapili ili ikatumike kuwalipia faini wafungwa waliopo magerezani pia zoezi hilo lifanywe na Misikiti ikiwezekana.
Mrema ameomba hili zoezi lifanyike kabla ya sikukuu ya Christmas na mwaka mpya ili wafungwa waweze kusheherekea sikukuu hizo na familia zao lakini pia anataka wafanyabiashara, wenye viwanda na wakulima wakubwa nao wachangie kwenye kampeni hiyo ya kuwakomboa wafungwa kutoka magerezani.
ULIKOSA HII SABABU ZA MREMA KUAMUA KWENDA KUMUONA RAIS MAGUFULI? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI