Moja ya stori iliyowahi kuwandikwa na Magazeti ya TZ wiki chache zilizopita ilikuwa na headline kuhusu ishu ya Ripoti ya Ukweli na Maridhiano ya TLP kutangaza kwamba imemsimamisha uanachama Mwenyekiti wa Chama hicho, Augustino Mrema ambae pia ni Mbunge wa Vunjo.. leo akapewa dakika zake chache kuwasha kipaza sauti ndani ya jengo la Bunge Dodoma.
“Wale wahuni waliotangaza wamening’oa TLP na kwamba mimi sio mwanachama wa TLP wala Mbunge wa Vunjo, naomba waandike wameumia”>>> Augustino Mrema.
“Mimi ndio Mbunge halali wa Vunjo ndoa hang’olewi mtu kule kwa greda wala katapila wala kwa winchi…” >>> Augustino Mrema.
Iko hapa sauti ya Mrema mwenyewe akiongea hayo Bungeni Dodoma leo.
Unahitaji chochote ninachokipata kisikupite? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.