Kama kawaida mtu wangu wa nguvu millardayo.com inakusafirisha kimawazo na kukufanya ujue mambo na tamaduni za nchi tofauti tofauti ili hata kama utaamua kwenda kutembea au kwenda kuweka makazi inabidi uvijue, November 6 millardayo.com inakukutanisha na Danny Mrwanda akieleza maisha ya Kuwait nchi ambayo amewahi kuishi.
Mshambuliaji huyo wa zamani wa Yanga, Simba na timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars Danny Mrwanda amewahi kucheza soka Kuwait mwaka 2008-2009 katika klabu ya Al Tadamon, Mrwanda ameeleza ugumu na sheria za nchi ya Kuwait, kama utakuwa unakumbuka vizuri Kuwait ni moja kati ya nchi zinazotumia sheria za dini ya kiislamu, tuliwahi kusikia kuwa ukikutana na mwanamke kimwili ambaye hamjaoana adhabu yako ni kupigwa mawe hadi kufa, Mrwanda anafunguka aliyokutana nayo.
“Kuwait haya masuala ya kuwa na mabinti ni vitu ambavyo haviruhusiwi kwa sababu hata Biblia na Quran inakataza kuzini, kwa mgeni ukitaka kwenda na mwanamke hadi uoneshe cheti cha ndoa, ukizini adhabu yake nasikia unatakiwa upigwe mawe hadi kufa, hata kuna wakati tuliwahi kuambiwa kuwa kuna binti alichomwa moto jangwani na wazazi wake baada ya kugundulika alikuwa amefanya mapenzi bila kuolewa” >>> Danny Mrwanda
Zaidi msikilize hapa Danny Mrwanda
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAMTWITTERFBYOUTUBE.