Mshambuliaji wa zamani wa klabu za Simba, Yanga na timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars Danny Mrwanda amekuwa bila timu inayoshiriki Ligi Kuu Tanzania bara kwa miezi kadhaa sasa toka pale mwanzoni mwa msimu huu alipoachwa na Yanga baada ya mkataba wake kumalizika.
Danny ambaye amewahi kucheza nje ya Tanzania kwa muda mrefu alikuwa na mpango wa kwenda Malaysia muda wowote kama mambo yake yangekuwa yameenda sawa, ila taarifa mpya kutoka klabu ya Maji Maji FC inayofundishwa na kocha raia wa Finland Mika Lonnstorm imethibitisha kufanya mazunguzo na wachezaji kadhaa akiwemo Danny Mrwanda na kufikia hatua nzuri.
Maji Maji FC wamethibitisha Danny Mrwanda kwenda kujiunga nao katika dirisha dogo la usajili ambalo litafunguliwa hivi karibuni kupitia kwa meneja wa timu hiyo Godfrey Ambrosi Mvula ambaye amethibitisha kuwafanyia majaribio wachezaji watatu kutoka Afrika Magharibi na kuwaomba Stand United iwauzie Hassan Dilunga kwa sababu wenyewe hawamtumii sana.
“Kuhusu suala la usajili kimsingi tumechukua wachezaji kama sita hivi watatu ni kutoka Ghana, Nigeria na Ivory Coast ambao ni wachezaji wanaofanya majaribio ila tumefanya mazungumzo na Danny Mrwanda yupo mbioni kuja lakini pia tumefanya mazungumzo na Stand United ya kumuomba Dilunga ambao wao hawamtumii sana” >>> Godfrey Ambrosi
Hii ni sauti ya meneja wa Maji Maji FC Godfrey Ambrosi Mvula
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAMTWITTERFBYOUTUBE.