Mkurugenzi wa Msama Promotion Alex Msama amepongeza juhudi za kamati ya chama cha Mapinduzi katika utoaji wa Elimu ya Uwekezaji kwa Watanzania, Kauli hiyo ameitoa leo Jumamosi August 12,2023 katika ofisi za Msama Promotion Biafra kinondoni Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari Alex Msama amesema “Naipongeza kamati ya chama cha Mapinduzi kwa kuendelea kutoa elimu ya uwekezaji katika nchi yetu Tanzania, Ni jambo jema watanzania wengi walikuwa wanapotishwa juu ya uwekezaji katika nchi yetu ya Tanzania lakini sasa watanzania washaanza kuelewa uwekezaji nchini Tanzania”
Aidha Msama ameshukuru Rais wa Tanzania Mama Dkt Samia Hassan Suluhu kwa kuendelea na juhudi ya kufanya kazi na kuwashawishi na wawekezaji kuja kuwekeza Tanzania.
Pia Mkurugenzi Msama amewaonya na kushangaa wanaobeza maendeleo ya nchi na wanaotaka kuhatarisha amani ya Tanzania “Wapo baadhi ya watu wanataka kuchafua amani ya nchi yetu, vyombo vya usalama naomba wawachukulie hatua ili kuhakikisha amani ya nchi yetu inaendelea kuwa imara”