Muimbaji wa muziki wa Gospel, Joyce Mwaikofu amesema muziki ni tiba ambayo inaweza ikamuondolea mtu msongo wa mawazo ambao unasababisha athari mbalimbali katika mwili.
Pia Mwaikofu ameiomba Serikali kutoa Elimu kwa wasanii wa muziki huo ili wajue umuhimu wa BASATA na COSOTA katika sekta ya muziki nchini.
Amesema fursa nyingi huwa zinakuja za nje na ndani Kupitia serikali na serikali haiwezi kutoa msaada kwa mtu mmoja wanaitaji waunde vikundi au vyama vya waimbaji Ili pindi fursa hizo zinapokuja ziwafikie Kwa wote na amesema waimbaji wa injili wapo nyuma sana na hawaelewi.
Akizungumza wakati akiutambulisha wimbo wake wa ‘Nitaifuta Machozi Hapo’ Katika kumbi za Center Point, Mwaikofu amesema muziki ni tiba kwani kuna watu wanapitia matatizo ya sonona na magonjwa mbalimbali lakini wanaponywa kupitia muziki.
“Changamoto zipo katika maisha yetu lakini muziki ni tiba na kama tunavyojua mtu unaweza ukawa mawazo na kusababisha mwili kupokea magonjwa na kinga zinashuka, kama utakuwa unaumwa hauwezi kufanya shughuli za maendeleo lakini kupitia mziki unaweza kujikuta unaponywa na vitu vingine vinaendelea kama kawaida,”.