Mkuu wa mkoa wa Tanga Dkt Batlida Buriani ameitaka bohari ya dawa nchini kuhakikisha vituo vyote vya afya mkoani humo vinakuwa na dawa muhimu ili kupunguza malalamiko ya wananchi ya ukosefu wa dawa .
Kauli hiyo imetolewa na Kaimu Mkuu wa mkoa ambaye ni Mkuu wa wilaya ya Tanga James Kaji wakati akifungua mkutano wa mwaka wa wadau wa MSD Kanda ya Tanga ambapo amesema kuwa katokana na uwekezaji uliofanywa na serikali ni muhimu kusiwepo na changamoto ya ukosefu wa dawa kwenye vituo.
“Serikali imeongeza bajeti ya afya hivyo ni jukumu la kuhakikisha mnasimamia bidhaa za afya Kwa kuzifikisha kwenye vituo vya kutolea huduma Ili kupunguza malalamiko ya wananchi ya ukosefu wa dawa pindi wanapokwenda kupata matibabu”amesema Kaimu Mkuu wa mkoa .
Hata hivyo Mkurungenzi ugavi na uendeshaji kutoka MSD makao makuu Victor Sungusia amesema kuwa bohari inaendelea na uboreshwaji wa huduma zake Ili kuhakikisha inaendelea kutoa huduma bora kwa wananchi.
Nae Meneja wa Kanda ya Tanga Sitti Abdurahman amesema kuwa Kwa kushirikiana na Wizara ya afya wamekuwa wakihakikisha vifaa vinavyohitajika vinapatikana na kusambazwa kwenye vituo vya afya .