Jeshi la Polisi Tanzania limewataka Watu wote wenye tabia ya kuvaa mavazi yanayofanana na sare za Majeshi ya Ulinzi na Usalama kinyume na sheria za Nchi, kuacha tabia hiyo mara moja kwani halitosita kuwakamata na kuwafikisha katika vyombo vya sheria.
Msemaji wa Jeshi la Polisi, David Misime amesema “Katika siku za karibuni kumeibuka makundi ya Watu, kampuni binafsi za ulinzi na baadhi ya Walinzi wa Viongozi wakivaa mavazi yanayofanana na sare za Majeshi ya Ulinzi na Usalama”
“ Sheria ya Kanuni ya adhabu sura ya 16 kifungu cha 178, kinakataza Mtu yeyote ambaye sio Askari wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama kuvaa sare za Majeshi, sheria ya Usalama wa Taifa ya mwaka 1970 kifungu cha 6, inakataza pia Mtu yeyote ambaye hatumikii Majeshi ya Ulinzi na Usalama ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wala Jeshi lolote lililowekwa kwa mujibu wa sheria kuvaa vazi rasmi la Jeshi lolote katika hayo yaliyotajwa au vazi lolote linalofanana na vazi rasmi la Majeshi hayo au kuwa na alama ya kiaskari au alama yoyote ya dhahiri ya hilo vazi rasmi au kumuajiri Mtu