Chama cha wananchi CUF kimekuwa na mgogoro wa uongozi tangu Profesa Lipumba ambaye July mwaka jana alijivua uenyekiti, atangaze nia ya kurejea.
Baada ya kuwepo mgogoro huo malalamiko na hoja ziliwasilishwa na baadhi ya wanachama na viongozi wa CUF kwa msajili wa vyama vya siasa kuhusu sintofahamu iliyopo katika chama cha CUF, kufuatia kujiuzulu kwa Prof. Ibrahimu Lipumba na hatua za kinidhamu zilizochukuliwa na kikao cha baraza kuu la uongozi la Taifa cha August 28 2016.
Msajili wa vyama vya siasa, Jaji Francis Mutungi baada ya upembuzi ametoa msimamo na mwongozo huu……..
'Baada ya upembuzi msimamo wangu ni kuwa Lipumba bado ni mwenyekiti halali wa CUF na waliofukuzwa, kusimamishwa ni wanachama halali'-Msajili
— millardayo (@millardayo) September 24, 2016
#UPDATE2 'Viongozi ambao uongozi wao uliathirika na maamuzi ya kikao cha baraza kuu la uongozi la Taifa bado ni viongozi halali CUF'-Msajili
— millardayo (@millardayo) September 24, 2016
'Viongozi CUF walioteuliwa na kikao cha baraza la uongozi wa Taifa ambao uteuzi wao ni batili wasijaribu kufanya shughuli yoyote':-Msajili
— millardayo (@millardayo) September 24, 2016
#UPDATE4 'Ktk kushughulikia mgogoro wa CUF, pamoja na kuangalia sheria inasemaje, nimesoma kwa makini maelezo ya pande zote mbili'-Msajili
— millardayo (@millardayo) September 24, 2016
ULIKOSA UCHAMBUZI WA MAGAZETI KUTOKA AYO TV, SEPTEMBER 24 2016? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI