Leo January 22, 2018 Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imesema inatarajia kutoa uamuzi kuhusu hati ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kuzuia dhamana kwa Mkurugenzi wa meli ya Lucky Shipping, Issa Haji na mwenzake February 5, 2018 wanaokabiliwa na kesi ya kupeperusha bendera ya Tanzania kimakosa.
Uamuzi huo unatarajiwa kutolewa na Hakimu Mkazi Mwandamizi, Victoria Nongwa kutokana na upande wa utetezi kuhoji uhalali wa kibali cha DPP kuzuia dhamana kwa washtakiwa hao.
Wakili wa utetezi, Dismas Raphael aliipinga hati hiyo ya dhamana kwa madai kuwa vitu ambavyo vinapaswa kuwepo kwenye hati ya zuio la dhamana kwa mujibu wa sheria kwenye hati hiyo havipo.
Pia amedai upande wa mashtaka hawajafafanua ni kwa nini usalama na maslahi ya Taifa yataingiliwa iwapo washtakiwa hao watapewa dhamana.
Wakili wa serikali, Wankyo Simon amedai hati hiyo ya zuio la dhamana ipo sawa, kwani endapo wakipewa dhamana basi maslahi na usalama wa Taifa utaingiliwa.
Mbali ya Haji, mshtakiwa mwingine ni mfanyabiashara Abdullah Hauga (73) ambaye ni Mkazi wa Mbezi Beach.
Washtakiwa wanakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi namba 2 ya mwaka 2018 ambapo wametenda makosa mawili.
Wanadaiwa kujihusisha na mtandao wa kiuhalifu ambapo walitenda kosa hilo kati ya July 19, 2017 na January 1, 2018 maeneo ya Dar es salaam.
Inadaiwa katika tarehe hizo walishauri, walitoa msaada na maelekezo ya kutenda kosa la jinai ambalo ni kupeperusha bendera ya Tanzania katika meli ya HUIHANG 68 ambayo awali iliitwa GREKO-02 bila kibali.
Pia kosa jingine la kupeperusha bendera ya Tanzania bila kibali, ambapo inadaiwa walilitenda kati ya July 19, 2017 na January 1, 2018.
Inadaiwa walipeperusha bendera ya Tanzania katika meli ya HUIHANG 68 ambayo awali ilijulikana kama GREKO-02.
BREAKING: Said amwaga machozi baada ya Scorpion kuhukumiwa miaka 7