Mshindi wa BSS msimu wa 14 ambaye alipatikana siku ya fainali ya January 27,2024, Razack Adam amekabidhiwa zawadi yake ya kiwanja chenye ukubwa wa square meter 500 kilichopo Vigwaza Mlandizi Mkoani Pwani.
Itakumbukwa siku ya fainali hiyo Razack alikabidhiwa hundi yenye thamani ya Tsh. milioni 30 na ramani ya kiwanja ambayo ndio leo amekabidhiwa rasmi kiwanja baada ya kukabidhiwa pesa zote milioni 30 siku moja tu baada ya kufanyika kwa fainali.
Baada ya kukabidhiwa kiwanja hicho kilichoahidiwa na moja ya Wadhamini wa shindano hilo Razack ameishukuru BSS kwa kuweza kupigania ndoto yake na kwa mara ya kwanza katika maisha yake ameweza kumiliki kiwanja chake mwenyewe na amesema ataanza ujenzi hivi karibuni.