Mshukiwa wa mauaji ya halaiki ya Rwanda Kabuga hayupo katika hali nzuri ya kiafya ili kushtakiwa-majaji
Share
1 Min Read
SHARE
Majaji katika mahakama ya umoja wa mataifa kuhusu uhalifu wa kivita wameamua kwamba mshukiwa wa mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 nchini Rwanda Félicien Kabuga, hayupo katika hali nzuri ya kiafya ili kushtakiwa.
Kesi ya Kabuga ilianza kusikilizwa katika mahakama ya The Hague mwezi Septemba mwaka uliopita.
Anashutumiwa kwa kufadhili wanamgambo wa Kihutu pamoja na kuhimiza matamshi ya chuki yatangazwe kwenye kituo chake cha redio, Radio Television Libre des Milles Collines (RTLM).
Mahakama hiyo Maalum ya Kimataifa yenye makao yake makuu mjini The Hague Uholanzi ilisema inaona kuwa “Félicien Kabuga hafai kushiriki kikamilifu katika kesi yake na huenda asipate utimamu wake katika siku zijazo”.
Imependekeza kubuniwe utaratibu “mbadala” wa kisheria ambao “unaendana na kesi kwa karibu iwezekanavyo, lakini bila uwezekano wa kuhukumiwa”.
Kesi ya Bw Kabuga, 90, ilisitishwa mwezi Machi kutokana na matatizo ya kiafya.
Alikamatwa huko Paris mnamo 2020 baada ya kukwepa kukamatwa kwa miaka 26.