Mamlaka ya Uturuki siku ya Alhamisi ilimkamata raia wa Iraq anayeshukiwa kuwa mwanachama wa kundi la kigaidi la Daesh/ISIS, kama ilivyothibitishwa na polisi.
Vikosi vya polisi vya kupambana na ugaidi vilimkamata mshukiwa, aliyetambuliwa na herufi za kwanza za A.A.T., katika operesheni katika mkoa wa Kirikkale.
Mshukiwa huyo alikuwa anatafutwa kwa notisi ya bluu iliyotolewa na Interpol.
Vilevile, vikosi vya usalama vya Uturuki vimewakamata watu wasiopungua 35 kote nchini kwa tuhuma za kuwa na uhusiano na kundi la kigaidi la Daesh/ISIS.
Takriban washukiwa 22 walizuiliwa mjini Istanbul, huku operesheni nyingine huko Izmir ikipelekea kuzuiliwa kwa washukiwa tisa, wote raia wa Syria. Sambamba na hayo vikosi vya usalama vya Uturuki vimewatia mbaroni watu wanne katika jimbo la Kayseri kwa tuhuma za kuwa na uhusiano na kundi la kigaidi la Daesh/ISIS.
Mnamo 2013, Türkiye ikawa moja ya nchi za kwanza kutangaza Daesh/ISIS kuwa shirika la kigaidi.