Baraza la Halmashauri ya wilaya ya Geita limewaonya Baadhi ya Viongozi katika kata watakao Kwenda kusimamia Mfuko wa Maafa ambao umeundwa kwa ajili ya kusaidia kutatua changamoto za Maafa wasiwe chanzo cha Mivutano katika vikao ambavyo vitaenda kutatua changamoto hizo.
Agizo hilo limetolewa na Mwenyekiti wa Baraza la Madiwani wilaya ya Geita , Charles Kazungu wakati wa uwasilishaji Taarifa mbalimbali za Miradi ya maendeleo katika kata huku akisema Tayari Baraza limepitisha kila Kata kupewa Mifuko mia moja ya Saruji ambayo itakwenda kusaidia kukarabati shule kongwe ambazo zitaezuliwa na Upepo hasa katika kipindi hiki cha Masika.
” Saruji hizi zitakazokuja tuko kwenye kipindi cha Mvua tukikaa tukaanza kubishana kwenye vikao vyetu vya kata saruji itaharibika ifike tuharakishe kupanga mikakati ni namna gani inakwenda kutumika nisingependa kupokea taarifa za kwamba kata fulani kuna saruji imeganda , ” Mwenyekiti Baraza la Madiwani Halmashauri ya wilaya ya Geita, Charles Kazungu.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Geita, Karia Magalo amesema wataendelea kushirikiana na Baraza la Madiwani katika kuhakikisha Mfuko wa Maafa unafanya kazi ipasavyo kama ambavyo vikao vimepitisha katika baraza la madiwani.
” Jinsi ambavyo katika Halmashauri yetu tumekuwa tukikumbwa na Maafa mbalimbali na jinsi tunavyoshirikiana lakini kwa upande wa Maafa kuna tunao utaratibu maalumu ambao unaanzia kule kwenye kata pale yanapotokea unaratibiwa na unafika mpaka kwa waziri Mkuu lakini maafa yanapotokea pia yanahusisha Mfumo wa kibajeti , ” Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Geita, Rajabu.
“Na kama ikitokea maafa vilevile utaratibu ni huo huo kwamba ni lazima urudishe kwenye ngazi hii pale inapopitisha na kulidhia ndipo tunapoweza kufanya utekelezaji kwa yale ambayo tayari Baraza lilikuwa limeshapitisha au kamati yetu ya fedha yanaendelea kutekelezwa kama vile Igate tumeambiwa tayari vifaa vinapelekwa , ” Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Geita, Rajabu.
Barnabas Mapande ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM wilaya ya Geita amelipongeza Baraza la Madiwani pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Karia Magalo kwa jinsi ambavyo wamekuwa wakishirikiana katika kutekeleza Miradi mbalimbali katika kata sambamba na utulivu wa Viongozi.
“Halmashauri yetu ya wilaya ni tulivu sana hongereni sana kwa utulivu ziko Halmashauri ni migogoro mpaka wanasimamishana na madiwani kwahiyo Mh Mwenyekiti kwa uongozi wako uongozi wa Mkurugenzi kwa umoja na mshikamano ndio unatufikisha hapa na penye utulivu ndio utaona shughuli za kimaendeleo , ” Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Geita, Mapande.